Posts

112. NILIKUPA WEWE MAISHA YANGU

NILIKUPA WEWE MAISHA YANGU 1.    Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   2.    Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   3.    Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   4.    Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   5.    Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   6.    Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.

113. NI MFALME WA MAPENZI

NI MFALME WA MAPENZI 1.    Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye.   2.    Kando ya maji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza.   3.    Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu.   4.    Uvulini mwa mauti, Sichi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu Wewe.   5.    Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa Wewe, yote naweza. Na msalaba mbele.   6.    Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako.

114. BWANA MUNGU, NASHANGAA KABISA

BWANA MUNGU, NASHANGAA KABISA 1.    Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote Viumbwavyo kwa uwezo wako. Chorus:   Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.   2.    Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia.   3.    Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno.   4.    Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo.

115. KILIMA KANDO YA MAJI

KILIMA KANDO YA MAJI   1.    Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana.   2.    Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu.   3.    Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima.   4.    Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu.   5.    Alijua peke yake Kufungua Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu.   6.    Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Nasi tumpende.

116. BWANA U SEHEMU YANGU

BWANA U SEHEMU YANGU 1.    Bwana u sehemu yangu,  Rafiki yangu, Wewe, Katika safari yangu,  Tatembea na wewe; Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Katika safari yangu,  Tatembea na wewe.   2.    Mali hapa sikutaka,  Ili niheshimiwe, Na yanikute mashaka,  Sawa sawa na wewe. Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Heri nikute mashaka  Sawa sawa na wewe.   3.    Niongoze safarini,  Mbele unichukue, Mlangoni mwa mbinguni,  Niingie na Wewe. Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Mlangoni mwa mbinguni,  Niingie na Wewe.

117. TUFANI INAPOVUMA

TUFANI INAPOVUMA 1.    Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu. Chorus:   Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.   2.    Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake.   3.    Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka.   4.    Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.

118. NI UJUMBE WA BWANA

NI UJUMBE WA BWANA 1.    Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! Wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   Chorus: Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   2.    Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu.   3.    Uzima wa daima,Aleluya ! Kwake Yesu utauona. Ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana.