113. NI MFALME WA MAPENZI

NI MFALME WA MAPENZI

1.  Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi.
Kunipoteza yeye.
 
2.  Kando ya maji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.
 
3.  Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.
 
4.  Uvulini mwa mauti,
Sichi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu Wewe.
 
5.  Waniandikia meza
Neema kwako tele.
Kwa Wewe, yote naweza.
Na msalaba mbele.
 
6.  Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.

Comments

Popular posts from this blog

118. NI UJUMBE WA BWANA