Posts

Showing posts from March, 2022

112. NILIKUPA WEWE MAISHA YANGU

NILIKUPA WEWE MAISHA YANGU 1.    Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   2.    Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   3.    Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   4.    Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   5.    Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   6.    Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.

113. NI MFALME WA MAPENZI

NI MFALME WA MAPENZI 1.    Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye.   2.    Kando ya maji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza.   3.    Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu.   4.    Uvulini mwa mauti, Sichi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu Wewe.   5.    Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa Wewe, yote naweza. Na msalaba mbele.   6.    Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako.

114. BWANA MUNGU, NASHANGAA KABISA

BWANA MUNGU, NASHANGAA KABISA 1.    Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote Viumbwavyo kwa uwezo wako. Chorus:   Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.   2.    Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia.   3.    Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno.   4.    Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo.

115. KILIMA KANDO YA MAJI

KILIMA KANDO YA MAJI   1.    Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana.   2.    Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu.   3.    Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima.   4.    Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu.   5.    Alijua peke yake Kufungua Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu.   6.    Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Nasi tumpende.

116. BWANA U SEHEMU YANGU

BWANA U SEHEMU YANGU 1.    Bwana u sehemu yangu,  Rafiki yangu, Wewe, Katika safari yangu,  Tatembea na wewe; Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Katika safari yangu,  Tatembea na wewe.   2.    Mali hapa sikutaka,  Ili niheshimiwe, Na yanikute mashaka,  Sawa sawa na wewe. Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Heri nikute mashaka  Sawa sawa na wewe.   3.    Niongoze safarini,  Mbele unichukue, Mlangoni mwa mbinguni,  Niingie na Wewe. Pamoja na Wewe,  Pamoja na Wewe, Mlangoni mwa mbinguni,  Niingie na Wewe.

117. TUFANI INAPOVUMA

TUFANI INAPOVUMA 1.    Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu. Chorus:   Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.   2.    Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake.   3.    Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka.   4.    Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.

118. NI UJUMBE WA BWANA

NI UJUMBE WA BWANA 1.    Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! Wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   Chorus: Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   2.    Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu.   3.    Uzima wa daima,Aleluya ! Kwake Yesu utauona. Ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana.

119. SI DAMU YA NYAMA

SI DAMU YA NYAMA 1.    Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa.   2.    Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ya thamani, Ni mwokozi kweli.   3.    Kwa imani yangu, Namshika yeye, Naziweka dhambi zangu Juu ya kichwa chake.   4.    Mzigo wa dhambi Sichukui tena, Ameuchukua yeye, Juu ya msalaba.   5.    Bwana Yesu ndiye, Mwokozi wa kweli Tumsifu siku zote, Twapata uhuru.

120. ENYI WANADAMU

ENYI WANADAMU 1.    Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema.   2.    Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba,mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka.   3.    Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru.   4.    Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake.   5.    Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atatujaza Tele furaha yake.

121. LIKO LANGO MOJA WAZI

LIKO LANGO MOJA WAZI 1.    Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi. Chorus: Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.   2.    Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini.   3.    Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena.   4.    Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima.   5.    Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa.

122. BWANA YESU

BWANA YESU 1.    Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu.   Chorus: Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame.   2.    Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, msalaba mabegani Kwa ajili ya watu.   3.    Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu.   4.    Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa.   5.    Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya!

123. NIMEKETI MIMI NILI KIPOFU

NIMEKETI MIMI NILI KIPOFU   1.    Nimeketi mimi nili kipofu Gizani nangojea macho; Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu, Ondoa dhambi zangu nzito. Chorus: Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.   2.    Tangu siku nyingi nimepofuka Natamani uso nikwone; Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka Sema neno, basi, nipone.   3.    Nimeketi mimi nili na giza, Nami ya kutumai sina; Ila nasikia kunong’oneza, “Kwake Yesu kuna k upona.”

124. MUNGU ULISEMA

MUNGU ULISEMA 1.    Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru.   2.    Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Nasi twakusifu, Twakushukuru.   3.    Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru.   4.    Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru.

125. ATI TWONANE MTONI

ATI TWONANE MTONI 1.    Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu. Chorus: Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.   2.    Tukitembea mtoni Na Yesu mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu.   3.    Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo.   4.    Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli.

126. NI MJI MZURI

NI MJI MZURI 1.    Ni mji mzuri, Mbali sana; Watu wanawiri Kama jua; Waimba kwa tamu, Tuna mwema Hakimu: Sifa na idumu, Kwake Bwana.   2.    Ni mji mzuri Twende sote! Una na fahari Msikawe! Raha tutaona, Dhambi hapana tena; Hatutaachana Siku zote.   3.    Ni mji mzuri; Macho yote Huko wanawiri Kama pete; Baba tutamwona, Tukifanywa tu wana; Tumo kupendana Naye sote.   4.    Ni mji mzuri; Tusipotee Na tuwe hodari, Tuupate! Tufunze, tutume Kwa taji na ufalme: Sifa na zivume Siku zote.

127. BWANA YESU ATAKUJA

  BWANA YESU ATAKUJA 1.    Bwana Yesu atakuja, Vumilia! Omba, ukiwa na haja, Vumilia! Mbinguni Mungu aliko, mwamini Mwokozi wako, Nawe utafika huko, Vumilia!   2.    Ikikucheka dunia, Vumilia! Mwovu atakuvizia, Vumilia! Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda, Roho yako, akupenda, Vumilia!   3.    Na ukiwa hatarini, Vumilia! Dhiki nyingi duniani, Vumilia! Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata, Na bwana hakutuficha; Vumilia!   4.    Adui wakikutana, Vumilia! Na ndugu wakikukana, Vumilia! Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha Mungu chini atashusha; Vumilia!   5.    Moyoni una majonzi, Vumilia! Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia! Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana Tena hatutaachana; Vumilia!

128. MMOJA APITA WOTE

MMOJA APITA WOTE 1.    Mmoja apita wote, Atupenda; Zaidi ya ndugu wote, Atupenda; Rafiki wa duniani, Wote hatuwaamini; Yesu kwa kila zamani, Atupenda.   2.    Kumjua ni uzima, Atupenda; Jinsi ajaavyo wema Atupenda; Yeye ametununua Kwa damu aliyomwaga, Dhambini kutuokoa, Atupenda.   3.    Sasa tunaye rafiki, Atupenda; Hupenda kutubariki; Atupenda; Twapenda kumsikia, Atwita kukaribia, Nasi tutamwamania, Atupenda.   4.    Husamehe Dhambi zetu, Atupenda; Hushinda adui zetu, Atupenda; Anatwonea huruma, Hatupati ila mema, Anatwongoza salama, Atupenda.

129. KARIBU NA WEWE

KARIBU NA WEWE   1.    Karibu na wewe, Mungu wangu Karibu zaidi, Bwana wangu Siku zote niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   2.    Mimi nasafiri Duniani, Pa kupumzika Sipaoni, Nilalapo niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   3.    Na kwa nguvu zangu Nikusifu; Mwamba, uwe maji Ya wokovu; Mashakani niwe Karibu na wewe; Karibu zaidi Mungu wangu.   4.    Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Zikikoma hapa Siku zangu, Kwa furaha niwe Pamoja na wewe, Karibu kabisa Mungu wangu.

130. NIONGOZE, BWANA MUNGU

NIONGOZE, BWANA MUNGU 1.    Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, Nilishe siku zote.   2.    Kijito cha maji mema, Kitokacho mwambani, Nguzo yako, moto, wingu, Yaongoza jangwani; Niokoe mwenye nguvu; Nguvu zangu na ngao.   3.    Nikikaribia kufa, Sichi neno lolote, Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote, Tutaimba sifa zako, Kwako juu milele.

131. PIGA SANA VITA VYEMA

PIGA SANA VITA VYEMA 1.    Piga sana vita vyema Kwa ushujaa daima, Yesu ndiye nguvu zako, Yesu ndiye kweli yako.   2.    Kaza mwendo, ushindane Angaza macho, umwone Yesu ndiye njia yako, Naye ndiye tuzo lako.   3.     Tupa kizito, simama, Tazama mbele, si nyuma; Ni yeye uzima wako, Naye ni kipendo chako.   4.    Tangamka, uamini Akushika mikononi Hageuki, akupenda, Kuwa naye una pia.

132. SAUTI SIKILIZENI

SAUTI SIKILIZENI 1.    Sauti sikilizeni Za waimbao juu, “Aleluya, Aleluya, Aleluya, mkuu!” Wako makundi-makundi Kama nyota wang’ara, Kwa makuti ya mitende, Na meupe wamevaa.   2.    Wazazi na manabii Wafanyaji wa njia; Mashahidi, waandishi, Nao wafalme pia! Mabikira kina-mama, Wajane wa kusali, Waimba wakikutana “Msifunu Imanweli”.   3.    Watu toka huzunini Wameosha na nguo, Ni kwa damu yake Yesu; Maonjo, mbali nao! Walitekwa, walikatwa Hata kwa misumeno, Kwao kifo na shetani Walishindiwa mno.   4.    Mungu mumo mwake Mungu, Nuru mumu mwa nuru, Kwa kufungamana mwako Tutaishi mahuru; Tujalize, Imanweli, Kujaa kwako wewe Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho, tunawe.