116. BWANA U SEHEMU YANGU

BWANA U SEHEMU YANGU

1.  Bwana u sehemu yangu, 
Rafiki yangu, Wewe,
Katika safari yangu, 
Tatembea na wewe;
Pamoja na Wewe, 
Pamoja na Wewe,
Katika safari yangu, 
Tatembea na wewe.
 
2.  Mali hapa sikutaka, 
Ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka, 
Sawa sawa na wewe.
Pamoja na Wewe, 
Pamoja na Wewe,
Heri nikute mashaka 
Sawa sawa na wewe.
 
3.  Niongoze safarini, 
Mbele unichukue,
Mlangoni mwa mbinguni, 
Niingie na Wewe.
Pamoja na Wewe, 
Pamoja na Wewe,
Mlangoni mwa mbinguni, 
Niingie na Wewe.

Comments

Popular posts from this blog

118. NI UJUMBE WA BWANA