120. ENYI WANADAMU

ENYI WANADAMU

1.  Enyi wanadamu mbona
Sana mwatanga-tanga,
Kama kondoo wanyonge,
Wasio na mchunga?
Yuko mchunga mmoja
Mwenye mapenzi mema;
Haya kutaneni kwake,
Atawachunga vyema.
 
2.  Mungu tunamwona kuwa
Mwenye uwezo wote;
Na nguvu zake zapita
Mawazo yetu yote:
Ni Baba,mapenzi yake
Ni makubwa hakika;
Hatuwezi kuyajua,
Na hayana mpaka.
 
3.  Rehema za Mungu nazo
Zina upana sana;
Kama huo wa bahari,
Mwisho wake hapana;
Haki yake ina mema,
Kwa hayo twashukuru,
Kwetu uko msamaha,
Furaha na uhuru.
 
4.  Mapenzi yake mapana,
Sisi hatuna cheo
Cha kutosha, nao moyo
Una wema upeo;
Ukombozi mwingi mno
Katika damu yake;
Sote twapata furaha,
Kwa maumivu yake.
 
5.  Yesu mkaribieni
Njoni msife myoyo;
Njoni kwake kwa imani,
Mema yake ni hayo;
Heri tuwe kama wana
Tushike neno lake,
Daima atatujaza
Tele furaha yake.

Comments

Popular posts from this blog

118. NI UJUMBE WA BWANA