136. MSIFUNI, YESU NDIYE MKOMBOZI

MSIFUNI, YESU NDIYE MKOMBOZI

1.  Msifuni, Yesu ndiye mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni, malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga achungavyo
Vivyo sisi kutwa atuchunga.
Msifuni mlio wake watoto
Msifuni aliye mchunga.
 
2.  Msifuni, Yesu ndiye mkombozi;
Akateswa tupate okoka;
Ndiye Mwamba, Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni kwake muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za baba yake Mungu.
Aliyefyolewa na kusulubiwa.
Msifuni ndilo letu fungu.
 
3.  Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni, enyi malango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.
Atakuja kuitawala nchi,
Yesu, Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli mwana wake Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

118. NI UJUMBE WA BWANA